<link rel="stylesheet" href="https://cdn.plyr.io/3.7.8/plyr.css" />
Rudi kwenye KatalogiFABaba Abrahamu
Baba Abrahamu ·ManuscriptImetafsiriwa kutoka Kiingereza

FA-01 Maisha ya Ibrahim: Muundo na Maudhui

Soma maandishi kamili

Inafungua hati...

Baba Abrahamu

­­

Maisha ya Abrahamu:
Muundo na Yaliyomo

Nukuu

Somo la 1

© 2020 Third Millennium Ministries

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuzalisha sehemu yoyote ile ya chapisho hili katika mtindo wowote (isipokuwa nukuu fupi kwa kusudi la mapitio, maoni, au taaluma) au kwa njia yoyote ile kwa kujipatia faida bila idhini ya mmiliki, Third Millennium Ministries, Inc., 316 Live Oaks Blvd., Casselberry, Florida 32707.

Toleo la Kiingereza

Isipokuwa imeoneshwa vinginevyo, Maandiko yote yamenukuliwa kutoka the HOLY BIBLE, NEW INTERNATIONAL VERSION. Toleo la © 1973, 1978, 1984, 2011 International Bible Society. Yametumika kwa idhini ya the Zondervan Bible Publishers.

Toleo la Kiswahili

Isipokuwa imeoneshwa vinginevyo, Maandiko yote yamenukuliwa kutoka The HOLY BIBLE IN KISWAHILI, UNION VERSION. PUBLISHED AS BIBLIA MAANDIKO MATAKATIFU. Toleo la © 1997, Bible Society of Tanzania.

Kuhusu Thirdmill

Hili ni shirika lililoanzishwa mnamo mwaka wa 1997. Thirdmill ni shirika la huduma ya Kiinjili ya Kikristo ambalo limejikita katika kutoa:

Elimu ya Biblia. Kwa Ajili ya Ulimwengu. Bila Malipo.

Lengo letu ni kutoa elimu ya Kikristo pasipo malipo kwa maelfu ya wachungaji na viongozi wa taasisi za Kikristo ulimwenguni kote. Mafunzo haya ni mahsusi kwa wachungaji ambao hawajapata mafunzo ya kutosha ya neno la Mungu yanayoendana na utumishi wao. Tunalifikia lengo hili kwa kuzalisha na kusambaza ulimwenguni kote mtaala wa seminari kwa njia mbalimbali za kimawasiliano kwa lugha ya Kiingereza, Kiarabu, Kimandarini, Kirusi, na Kihispania. Mtaala wetu unaendelea kutafasiriwa katika lugha nyingi mbalimbali kupitia washirika wetu katika huduma hii. Mtaala wetu unajumuisha picha za video, maelekezo yaliyochapishwa/nukuu, ambayo yote yanapatikana kwenye intaneti. Mtaala huu umeandaliwa ili uweze kutumiwa katika mashule, vikundi, na watu binafsi, kwa njia zote mbili; njia ya mtandao na katika jumuia ndogondogo za kujifunza Neno la Mungu.

Kwa miaka mingi, tumeandaa masomo na maudhui ya kiwango cha juu sana na kuyatoa kwa njia rahisi na kupunguza gharama za masomo. Waandishi na wahariri wetu ni wabobezi katika Theolojia. Pamoja na ukweli huo, wao pia ni wazungumzaji wa lugha husika. Masomo yetu yameandaliwa na wanazuoni waliobobea katika Theolojia, wakufunzi wa seminari, na wachungaji wa makanisa kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Pamoja na hayo, wabunifu wetu wa picha, wachoraji wa vielelezo na wazalishaji wa Makala wanafanya kazi zao kwa viwango vya juu sana.

Ili kutimiza lengo letu la usambazaji na kuwafikia watu wengi zaidi, Thirdmill imebuni mbinu ya kushirikiana na makanisa, seminari, shule za Biblia, wamishenari, watangazaji Wakristo na wahudumu wa huduma za televisheni, na mashirika mengine. Ushirika wa jinsi hii umewezesha usambazaji wa masomo yetu kwa haraka na kuwafikia viongozi mbalimbali, wachungaji, na wanafunzi wa seminari. Pia tovuti yetu hutumika kama jukwaa la usambazaji na utoji wa Elimu ya ziada ili kukamilisha masomo yetu. Kupitia tovuti yetu Mkristo yeyote yule anaweza kuanzisha darasa la watu wenye lengo la kujifunza Neno.

Thirdmill inatambuliwa nchini Marekani na taasisi ijulikanayo kwa jina la IRS kuwa ni shirika la 501(c) (3). Hii ina maana kuwa shirika linaendeshwa kwa kutegemea michango kutoka makanisani, mashirika, biashara, na watu binafsi. Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma yetu, na kujifunza namna ambavyo unaweza kushiriki, tafadhali tembelea tovuti yetu: www.thirdmill.org

Yaliyomo

UTANGULIZI 1

MUUNDO WA KIFASIHI 2

Mwanzo 2

Abrahamu 3

Vitengo vya Msingi 3

Mpangilio 5

MADA KUU 6

Kifungu Muhimu 7

Utangulizi 7

Sehemu ya Kwanza 8

Sehemu ya Pili 8

Yanayofunuliwa 9

Neema ya Kiungu 9

Uaminifu wa Abrahamu 10

Baraka kwa Abrahamu 11

Baraka kupitia Abrahamu 12

HITIMISHO 14

UTANGULIZI

Sote tunafahamu kuwa kuna tofauti nyingi miongoni mwa mataifa hapa duniani. Kila taifa lina jiografia yake, jamii yake na tamaduni za kipekee. Lakini kuna jambo moja ambalo kw kawaida linafanana katika nchi nyingi: sote tuna hadithi ya kipekee ya jinsi mataifa yetu yalivyoanza. Wengi wetu tunapenda kusikia kuhusu jinsi watu walioanzisha nchi zetu walivyojitoa mpaka kupata mafanikio. Na tunaimba nyimbo za kusifu ushujaa wao. Swali la msingi ni, kwanini tunatunza na kutangaza habari hizi za asili mara kwa mara? Kwanini jambo hili ni muhimu karibu katika kila utamaduni wa mwanadamu?

Zipo sababu kama mbili hivi za kufanya hivyo. Kwanza, tunazungumzia asili ya mataifa yetu ili kuyaendeleza mawazo na mambo yaliyopita. Tunataka watoto wetu wakumbuke asili zao, na wapi walikotoka. Lakini kwa upande mwingine, tunataka pia tukumbuke maadili yaliongoza mataifa yetu wakati uliopita ili tuweze kupata mwelekeo wa wakati ujao.

Hali kadhalika, hii ilikuwa kweli kwa watu wa Mungu pia katika Agano la Kale. Waisraeli wa kale walitunza historia kuhusu mwanzo wao na kuziendeleza kizazi hadi kizazi kwasababu hizo mbili. Walitunza historia kuhusu siku za mababu zao, na kuyakumbuka matukio ya zamani ili mafanikio makubwa yaliyopita yasisahaulike. Lakini pia walizisimulia habari hizi zilizopita kutoka kizazi hadi kizazi ili kujikumbusha ni upande gani wanapaswa kuelekea kwa wakati ujao.

Hili ni somo letu la kwanza katika mfululizo wa masomo yahusuyo, Baba . Katika mfululizo huu tutachunguza simulizi ambazo Waisraeli wa Kale walizisimulia kuhusu , baba yao mkuu. Na pia tutaona kuwa Musa aliandika habari hizi katika kitabu cha Mwanzo ili Waisraeli katika siku zao waweze kukumbuka yaliyopita, na kwa hiyo waweze kuuelewa kwa wazi zaidi wakati ujao ambao Mungu alikuwa nao katika mawazo yake kwa ajili yao.

Hili ni somo la kwanza kati ya masomo matatu katika mfululizo huu, na tumeliita, “Maisha ya : muundo na yaliyomo”. Katika somo hili tutaanza na maelezo ya jumla ya maisha ya kwa kuangalia kwa makini muundo na yaliyomo katika sura za kitabu cha Mwanzo ambazo zinazungumzia kumhusu yeye. Ni jinsi gani Musa aliunda habari za maisha ya ? Ni mambo gani ambayo ni makuu na muhimu katika sura hizi?

Tutachunguza muundo na yaliyomo katika maisha ya katika sehemu mbili: kwanza, tutaangalia kielelezo kinachoaminika katika mambo yaliyoandikwa. Na pili, tutachunguza mada kuu ndani ya sura hizo. Tuanze kuangalia kwanza kuhusu kielelezo kinachoaminika katika maisha ya .

MUUNDO WA KIFASIHI

Kila mara tunapotazama sehemu za Maandiko kama maisha ya ambayo yanasimulizi au habari, lazima tukumbuke kuwa waandishi wa Biblia walifanya zaidi ya kuandika tu ukweli wa mambo yaliyotokea zamani za kale. Kwasababu Roho Mtakatifu aliwavuvia wawe wazungumzaji wa Mungu. Hivyo, habari walizoziandika zilikuwa za kweli kabisa. Lakini Roho Mtakatifu aliwavuvia pia kuandika mahitaji ya watu walio waandikia, kwahiyo waandishi wa Biblia pia waliandika kupitia historia ya wasomaji wao. Kwa makusudi waliandika habari hizo, ili habari hizo ziwe sambamba na maisha ya watu waliozipokea.

Tunapoangalia habari za maisha ya katika kitabu cha Mwanzo, tunaweza kuwa na uhakika kuwa, habari hizi hazikosei kusema yaliyotokea hasa katika maisha ya . Lakini ili kuelewa jinsi habari hizi zilihusisha maisha ya watu wa asili ya wasomaji wa Musa, lazima pia tuwe na tahadhari ya jinsi kitabu cha Mwanzo kinaonesha maisha ya . Njia mojawapo ya kutuwezesha kuelewa jinsi anavyooneshwa ni kwa kuchunguza kielelezo cha wazi cha maisha ya katika kitabu cha Mwanzo.

Tutachunguza kielelezo cha wazi cha maisha ya katika hatua mbili. katika nafasi ya kwanza, tutaonesha mtazamo wa jumla wa kitabu cha Mwanzo, na tutaona jinsi habari za zinavyoingia katika mtazamo mkubwa katika Mwanzo. Na sehemu ya pili, tutaangalia muundo wa habari ambazo zinalenga maisha ya . Tuanze na kuangalia mtazamo wote wa kitabu cha Mwanzo.

Mwanzo

Kwa karne mbalimbali, watafsiri wengi wameelewa kinachotawala muundo wa Mwanzo katika njia tofauti. Mojawapo ya kuangalia ni kugawanya Mwanzo katika sehemu kumi kufuatana na kila tunachosema kurudiwa kwa vile vinaitwa “vizazi” au “toledot” sehemu zilizoenea kitabu chote cha Mwanzo. Na lazima tukubali kuwa, kuna faida fulani katika mtazamo wa sehemu hii kubwa. Lakini tumeshauri katika mifululizo mingine kuwa, ina msaada mkubwa kufikiria Mwanzo katika sehemu tatu kubwa: wakati wa zamani sana wa historia ya Mwanzo katika sura ya 1:1-11:9; wakati wa mapema wa zamani wa historia ya mababu katika sura ya 11:10-37:1; na baadaye historia ya wazee katika sura ya 37:2-50:26.

Historia ya zamani katika Mwanzo sura ya 1:1-11:9 ilionesha kufunua ukweli wa asili ya ulimwengu. Inazungumzia juu ya uumbaji, kuharibiwa kwa uumbaji, na kuujenga upya uumbaji, kupitia gharika kuu la ulimwengu. Na inashikilia pamoja kifungu cha wazi katika njia zinazofanana na sehemu za mambo mengi ya kale karibu na historia za mashariki ya zamani.

Baadaye historia ya wazee katika sura ya 37:2-50:26 inazungumzia habari ya Yusufu. Inaanza na mgongano kati ya Yusufu na kaka zake, halafu inaelekea kuinuka kwa Yusufu katika utawala huko Misri na mapatano ya Yusufu na kaka zake pale mwisho. Watafsiri wengi wamefafanua sehemu hii kubwa kama aya ya historia ya riwaya “novella” kuhusu Yusufu.

Kati ya sehemu hizi za mwanzo na mwisho katika sura ya 11:10-37:1. Sehemu hizi zina historia ya mababu wa zamani, mkusanyiko wa historia kuhusu mababa wa kwanza, mkusanyiko wa habari kuhusu mababa wa taifa la Israeli. Katika mfulululizo huo, tunahusika na sehemu moja ya sehemu ya kati ya kitabu cha Mwanzo.

Katika mtazamo wa jumla, historia ya mapema ya wazee inagawanyika katika sehemu mbili: Maisha ya Abrahamu katika sura ya 11:10-25:18 na maisha ya Yakobo katika sura ya 25:19-37:1. Sasa mgawanyiko huu wa sehemu mbili inaweza kuwa ya kushangaza, kwanza kwa sababu katika Maandiko tunasikia mara kwa mara kutajwa wazee watatu wa mapema: Abrahamu, Isaka, na Yakobo. Kwahiyo, tunaweza kutegemea wazi kuwa muundo wa sura hizi kuwa na sehemu tatu pia, kwanza ikizungumzia kuhusu Abrahamu, na baadaye kuhusu Isaka, na baadaye kuhusu Yakobo. Lakini katika uhalisia, hakuna katika sehemu ya historia ya mapema iliyoshughulikiwa kwa Isaka kama mhusika mkuu. Badala yake, inatumika kama umbo la mpito. Maisha yake yanazungumziwa kwanza kama sehemu ya maisha ya Abrahamu na baadae sehemu ya maisha ya Yakobo. Na kwa matokeo, historia ya mapema ya wazee inagawanyika hasa katika sehemu mbili kuu: Maisha ya Abrahamu na baadae maisha ya Yakobo. Wajibu wetu katika mfululizo wa sehemu ya nusu ya kwanza ya kipindi cha wazee, ni maelezo ya Musa ya Baba . Kwa hiyo, tuangalie mtazamo wa makini katika muundo wa maisha ya kama ilivyoelezwa katika Mwanzo 11:10-25:18.

Abrahamu

Sasa, kuwa tumeona na kugundua mahali ambapo maisha ya yanaungana katika kutawala muundo wa Mwanzo, tunaweza kuangalia kile kinachotuhusu katika sehemu inayofuata: muundo wa maisha ya katika Mwanzo 11:10-25:18. Kuchunguza muundo wa maisha ya , tutaangalia ndani ya sura hizi katika ngazi mbili: kwa upande mwingine, tutatambua tu zile sehemu za msingi au matukio ya maisha ya , na kwa upande mwingine, tutachunguza jinsi matukio fulani yalivyopangwa katika picha ya tuliyonayo katika Mwanzo. Tuanze kutambua sehemu za msingi au matukio ya maisha ya .

Vitengo vya Msingi

Musa aliandika kuhusu Maisha ya katika sehemu za msingi kumi na saba:

  1. Ya kwanza, Ukoo wa ulipendelewa (sura ya 11:10-26), kizazi kinachofafanua familia ya Abrahamu na urithi wake.
  2. Sehemu hii inafuatiwa na maelezo ya kuanguka kwa baba yake (katika sura ya 11:27-32), ya pili ni kizazi kinacho fafafanua safari ya na baba yake Tera.
  3. Kuhamia kwa kule Kaanani (sura ya 12:1-9), Habari ya kwanza ya kuitwa kwa na safari ya kwenda kwenye Nchi ya Ahadi
  4. Ukombozi wa kutoka Misri (sura ya 12:10-20), wakati ambao alisafiri Misri na Mungu alimkomboa kutoka huko.
  5. Mgongano wa na Lutu (sura ya 13:1-18), mapambano kati ya watu wa na wale wa Lutu.
  6. kumwokoa Lutu (sura ya 14:1-24), wakati alipopigana na na kumwokoa Lutu kutoka kwa Wafalme waliomteka.
  7. Agano la Abrahamu na ahadi (sura ya 15:1-21), maelezo ya Ahadi ya Mungu kumhakikishia Abrahamu kuwa atakuwa na ukoo mkubwa na makao ya kudumu ya nchi yake.
  8. Kushindwa kwa Abrahamu pamoja na Hagai. (sura ya 16:1-16), Ni wakati Abrahamu alipopata mtoto, Ishimaeli, na mtumishi wa Hagai mtumishi wake.
  9. Mahitaji ya ahadi za Abrahamu (sura ya 17:1-27), maelezo ya Ahadi ya Mungu ambayo yanamkumbusha Abrahamu ulazima wa uaminifu kwa amri za Mungu.
  10. Sodoma na Gomora (sura ya 18:1-19:38), Habari ya kuharibiwa kwa Sodoma na Gomora na Lutu kuokolewa katika uharibifu huo.
  11. Maombezi ya Abrahamu kwa Abimeleki (sura ya 20:1-18), wakati ambao Abrahamu alimwombea Abimaleki Mfilisti.
  12. Watoto wa Abrahamu Isaka na Ishimaeli (sura ya 21:1-21), habari ya kuzaliwa kwa Isaka na kufukuzwa kwa Ishimaeli kutoka kwa familia ya Abrahamu.
  13. Mapatano ya Abrahamu na Abimaleki (sura ya 21:22-34), wakati ambao Abrahamu aliingia katika makubaliano na Abimaleki juu ya maji na uhalali wa nchi.
  14. Kujaribiwa kwa Abrahamu (sura ya 22:1-24), kisa kinachojulikana ambacho Mungu alimwita Abrahamu kumtoa sadaka mwanaye Isaka.
  15. Mali ya Abrahamu (sura ya 23:1-20), habari ya kifo cha Sara na kununuliwa kwa sehemu ya kumzikia.
  16. Mke wa Abrahamu na mtoto Isaka (sura ya 24:1-67), wakati Rebeka alipokuwa mke wa Isaka.
  17. Na mwisho, kifo cha Abrahamu na urithi (sura ya 25:1-18), habari ya kupita kwa Abrahamu na maelezo ya kizazi hicho.

Kama tunavyoweza kuona, habari ya mke wa Abrahamu inafuata kwa msingi wa matukio kama yalivyotokea katika maisha yake. Habari zake zinaanza wakati akiwa kijana chini ya mamlaka ya baba yake, na yanaishia na Abrahamu amekuwa mzee na kufa. Katika matukio, kuna njozi mbaya na muunganiko wa kati ya matukio ya wazi ya maisha ya Abrahamu. Lakini kwa kulinganisha na sehemu nyingine za Agano la Kale, habari za maisha ya Abrahamu zina mfululizo wa mambo kumi na saba yanayojitegemea. Kila moja ya tukio lililenga kusimulia matukio katika maisha ya Abrahamu yanayofundisha masomo halisi kwa Musa na asili ya hadhara ya Waisraeli. Kama Musa alivyowaongoza kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi, kila tukio katika haya lilitoa fundisho katika maisha yao, na kama yanavyotoa mafundisho kwetu tunavyoishi katika maisha yetu leo.

Baada ya kutambulisha matukio ya msingi ya maisha ya Abrahamu, sasa tuchunguze jinsi sehemu hizi zinashikamana pamoja. Ni namna gani habari za Abrahamu zimeungana? Ni kwa mantiki gani inayozipanga pamoja? Weka tu, matukio ya maisha ya Abrahamu yanaunganika kupitia mada maalumu, na muunganiko huu unaunda chaguzi tano zilizo sawa au zilizo na hatua zenye kulingana.

Mpangilio

Kwanza, kama tunavyoweza kutegemea katika mwanzo wa maisha ya wazee, maelezo ya Musa yanaanza na historia ya nyuma ya Abrahamu na uzoefu wake na Mungu. Sehemu hii inajumlisha: ukoo wa Abrahamu uliopendelewa, baba yake aliyeshindwa, na uhamiaji wake kwenda Kanani. Sura hizi zinaeleza jinsi Abrahamu alivyoingia katika uhusiano maalumu na Mungu kwa kuangalia historia ya nyuma ya historia ya familia na mwanzo wa kuhamia Nchi ya Ahadi.

Kusanyiko la pili la matukio katika maisha ya Abrahamu yanajikita katika sehemu ya mapema ya maisha ya Abrahamu, pamoja na uhusiano na watu wengine katika sura ya 12:10 hadi 14:24. Inajumlisha kuokolewa kutoka Misri, mgongano wake na Lutu, na alivyomuokoa Lutu. Matukio haya matatu yanashikamana pamoja kwasababu yanaunganisha kimsingi kukabiliana na ushirikiano na wawakilishi wa makundi kadhaa ya watu. Katika sura hizi, wazee kimsingi walishughulika na Farao wa Misri, na mpwa wake Lutu, akivamiwa na Wafalme, Mfalme wa Sodoma na Melchizedeki mfalme wa Yerusalemu.

Sehemu ya tatu ambayo ni ya katikati ya maisha ya Abrahamu kwa Agano la Abrahamu la uhusiano na Mungu katika sura ya 15:1–17:27. Sehemu hii ya maisha ya wazee ina matukio matatu: Ahadi za Agano la Abrahamu, kuanguka kwa Abrahamu na Hajiri, na mahitaji ya Agano la Abrahamu.

Sehemu ya nne, ambayo inaonekana katika sura ya 18:1–21:34, inarudi kwa majina ya watu wengine. Sura hizi zinashikilia pamoja kimsingi kwa sababu zinazingatia mahusiano ya Abrahamu na makundi ya watu wengine. Sura hizi zinaelezea Abrahamu katika kuhusiana na Sodoma na Gomora. Tunakuta mahusiano ya Abrahamu kwa Abimaleki, Abrahamu na uhusiano na Isaka na Abimaleki, Abrahamu katika uhusiano na Isaka na Ishmaeli, na mapatano ya Abrahamu na Abimaleki. Matukio haya manne yanaonesha zaidi jinsi wazee hawa walihusiana na Lutu na familia yake, pamoja na jinsi alivyohusiana kwa watu wa Sodoma na Gomora na kwa Abimaleki Mfilisti.

Kama tunavyoweza kutegemea, sehemu ya tano na ya mwisho ya maisha ya wazee hawa katika sura 22:1–25:18, inashughulika na mambo kuelekea mwisho wa maisha ya Abrahamu, hasa kizazi chake na kifo chake. Inaeleza jinsi Abrahamu alivyojaribiwa. Inaelezea Abrahamu alivyonunua sehemu ya maziko. Inaelezea jinsi Abrahamu alivyompatia mke mwanaye Isaka. Na inaelezea pia kifo cha Abrahamu. Sura hizi zinalenga kwa mke wa Abrahamu Sara na mtoto wake Isaka (mrithi wa kweli wa Abrahamu), ikiwapa heshima juu ya wake wengine wa Abrahamu na watoto wao.

Kwasababu matukio ya maisha ya Abrahamu kwa kiasi fulani yanajitegemea kwa kila moja, wakati kwa mara ya kwanza watu walisoma juu ya Abrahamu, mara nyingi wanakuwa na wazo la kutangatanga bila kuwa na lengo kutoka tukio moja hadi lingine. Wanazisoma habari za Abrahamu kama vile Musa alivyoyataja matukio haya na mawazo bila kuyapanga. Lakini haidhuru ya mtazamo huu, habari za maisha ya Abrahamu kwa kweli zimewekwa katika vifungu au makundi ya matukio yanayohusiana na mada za katikati. Hatua zetu tano za kawaida zinaainisha na kugundua kuwa Musa alipanga ni nini ambacho alikuwa anataka kusema kuhusu Abrahamu. Katika kipimo kikubwa zaidi maelezo ya maisha ya Abrahamu yanachukua nafasi ya matukio ya ulinganifu. Kila sehemu inalingana na kuhusiana na sehemu katika tukio.

Katika sura ya 11:10–12:9, tunakuta kipaumbele kinaelenga juu ya historia ya nyuma ya familia ya Abrahamu katika mahusiano ya mwanzo na Mungu. Katika kulinganisha uwiano pamoja na uhusiano wa mwanzo, mambo ya kufunga katika sura ya 22:1–25:18 yanatupa angalizo la mwisho wa miaka ya Abrahamu kwa kizazi chake.

Zaidi ya hapo, sehemu ya pili ya maisha ya Abrahamu ya matukio ambayo kimsingi yanaonesha mahusiano ya Abrahamu na watu kutoka makabila na mataifa mengine. Na kwa ulinganifu wa kuzunguka, kurudi katika mada zinazofanana tulizoziona katika sehemu ya pili, sehemu ya nne ya maisha ya Abrahamu inarudi katika lengo la mifano zaidi ya makabiliano ya Abrahamu na wengine.

Mwisho, katika maisha ya katikati ya Abrahamu, kuna sura tatu za msingi ambazo zinalenga hasa agano la Abrahamu na Mungu. Sura hizi zinaunga nguzo ya katikati ya maisha ya Abrahamu inayoelezea matukio ya msingi wa uhusiano wa agano ambalo Abrahamu na vizazi vyake walilokuwa nalo na Mungu.

Taswira ya sura hizi inaonesha kuwa Musa kwa uangalifu aliweka kwa makini maelezo yake. Alijenga picha ya wazi ya wazee wa kwanza wa Israeli ili kuvuta angalizo kwa mitazamo fulani katika maisha yake: Uchaguzi wa Abrahamu kwa baraka ya ukweli wa urithi, Uhusiano wa Abrahamu wa mapema na baadaye mahusiano, na Agano la uhusiano wa Abrahamu na Mungu. Na kama tutakavyoona, hili lengo la wazi lilikuwa limetolewa kusema mahitaji ya Waisraeli ambao Musa aliandika habari hizi wakiwa wasomaji wa kwanza. Maisha ya Abrahamu yaliwafundisha Waisraeli jinsi watakavyofuata hatua za Abrahamu kama Musa laivyowaongoza kwenda kwenye Nchi ya Ahadi. Na tunapokaribia sehemu hii ya Mwanzo, tutaona umuhimu wa ubunifu huu kwa muda na makusudi yake.

Baada ya kuona wazi ubunifu unaotawala maisha ya Abrahamu, tunapaswa kugeukia mada ya pili ya somo juu ya muundo na yaliyomo katika maisha ya Abrahamu: Mada kuu za Mwanzo sura ya 11:10–25:18. Ingawaje kuna njia nyingi za kuelezea yaliyomo katika sura hizi, tutaona kuwa muhutasari tulioushauri unalingana na mada maarufu katika sura hizi.

MADA KUU

Napenda kusema kuwa, ni vigumu kuelezea mada kuu katika sehemu yoyote ya Maandiko ambayo ni ndefu na yenye matukio yaliyochangamana kama maisha ya Abrahamu. Haiwezekani kutaja kila kusudi au neno kuu ambalo linaonekana katika sura hizi. Lakini inawezekana kugawanya mkusudi kadhaa ambayo ni maarufu kuliko mengine. Na kama tutakavyoona, hizi mada kuu katika sura hizi zinaunganisha habari za maisha ya Abrahamu, na zinatusaidia kuelewa mawazo makuu ambayo Musa alitaka wasomaji wake wa asili wa Kiisraeli wapate kutoka katika maisha ya Abrahamu. Na zaidi ya hapo, tunaweza pia kuona, katika mada hizi kuu, ni nini Mungu anakusudia sisi kujifunza kupitia sehemu hii ya Maandiko.

Tuatangalia katika mada kuu za maisha ya Abrahamu katika njia mbili: Ya kwanza, tutapima kifungu cha msingi ambacho kinatutambulisha mada kuu nne za maisha ya Abrahamu. Na pili, tutachunguza njia za mada na kuzifungua kupitia sura za maisha ya Abrahamu. Tugeukie kwanza katika vifungu muhimu vinavyoelezea habari za Abrahamu.

Kifungu Muhimu

Utakumbuka kuwa, katika ufunguzi wa habari za maisha ya Abrahamu tumeona wito wa Mungu kwa Abrahamu katika Mwanzo sura ya 12:1-3. Wakati Abrahamu akiishi katika Uru ya Mesopotamia, Mungu alimwita Abrahamu aende kwenye Nchi ya Ahadi. Kwa miaka mingi sasa, wafasiri wametambua kuwa vifungu hivi vinatambulisha mambo kadhaa yenye makusudi muhimu yaliyopatikana katika habari kubwa za maisha ya Abrahamu. Sikiliza ni nini, Musa aliandika katika vifungu hivi:

Bwana akamwambia Abram, “Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” (Mwanzo 12:1-3).

Vifungu hivi vitatu vimejaa maneno muhimu na vinaweza kufupishwa katika njia nyingi tofauti. Katika kiwango cha kisarufi, zinaanza na utangulizi katika sehemu ya kwanza ya vifungu hivyo, 1. Badaye zinaendelea na maneno ya Mungu kwa Abrahamu, ambayo yanagawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza, katika sehemu ya nusu ya kwanza ya kifungu cha 1 hadi sehemu ya 2 ina amri inayofuatiwa na amri zilizohuru zinazojieleza. Katika kuangalia vifungu hivi vitatu vya Mwanzo 12:1-3 tunaweza kupata mawazo muhimu ya kifungu hiki.

Utangulizi

Sikiliza kwanza njia rahisi ya Musa alivyotambulisha maneno ya Mungu kwa Abrahamu katika kifungu cha 1:

Bwana akamwambia Abramu (Mwanzo 12:1).

Watafasiri walio wengi wanakubaliana kuwa, kitenzi katika mstari huu ingepaswa kutafsiriwa kama “Bwana alisema” Badala ya “Bwana akamwambia”. Tafsiri hii ni ya muhimu kutokana na hotuba ya Stephano katika 7:2-4, Abrahamu alipokea wito wake katika Uru kabla ya baba yake Tera kufariki katika sura ya 11:32 na badaye tunajifunza katika Mwanzo 12:1 kuwa Mungu alimwita Abramu. Kwa sababu hii, Mwanzo 12:1 inawakilisha usemi wa nyuma, unaopaswa kutafsiriwa, Bwana alisema”. Kifungu hiki kinakumbushia wakati wa mapema kabla ya Abrahamu hajaanza kufanya chochote katika mwitikio wa Mungu, zamami kabla ya kuanza kwenda kwenye Nchi ya Ahadi.

Sehemu ya Kwanza

Kwa kupitia utangulizi huu, tunaweza kuendelea na nusu ya kwanza ya maneno ya Mungu kwa Abrahamu. Nusu ya kwanza inaanza na kitenzi cha amri, inayoonesha amri. Katika Mwanzo 12:1 tunasoma maneno haya:

Bwana akamwambia Abram, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha (Mwanzo 12:1).

Kama tunavyoweza kuona, sehemu hii inaanza na amri, “Toka” (au kama NIV inavyolifafanua “ondoka … na uende”). Mungu alimwamuru Abrahamu kutoka kwenda katika nchi ya Kanani. Hii ndiyo amri ya kwanza na ya msingi Mungu aliyompa Mzee huyo.

Baada ya amri ya kuondoka kwenda kwenye Nchi ya Ahadi, sehemu ya kwanza ya maneno ya Mungu kwa Abrahamu inagawanyika katika sehemu tatu zilizohuru na zinaoonesha vitenzi vinazojitegemea katika sehemu ya kwanza ya kifungu cha 2. Angalia tena Mwanzo 12:2:

Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka (Mwanzo 12:2).

Maneno haya yanalenga baraka ambazo Mungu alizitoa kwa Abrahamu alivyomwita. Kwanza, Mungu alisema atamfanya Abrahamu taifa kubwa. Pili, aliahidi kumbariki Abrahamu kwa mafanikio. Na tatu, alisema angelikuza jina la Abrahamu na vizazi vyake.

Sehemu ya Pili

Sasa tuangalie sehemu ya nusu ya pili ya maneno ya Mungu kwa Abrahamu. Ingawa tafsiri nyingi za kisasa haziwezi kutuwezesha kuiona, sehemu ya pili ya maneno ya Mungu kwa Abrahamu inaenda sambasamba na mpangilio wa sarufi ya sehemu ya nusu ya kwanza. Inaanza na amri ikifuatiwa na ufafanuzi wa vitenzi vitatu vilivyo huru katika Mwanzo 12:2-3 tunasoma maneno haya:

Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” (Mwanzo 12:2-3).

Kitenzi cha Kiebrania kilichotafsiriwa hapa, “Utakuwa baraka”, ni amri katika umbo, na pengine imeumbwa kwenda sambamba na umbo la amri. “toka” katika kifungu cha 1. Lakini ulazima huu haufanyi kazi kama amri. Inaweza kutafsiriwa katika njia nyingi kama: “na utakuwa baraka” au “na pengine utakuwa baraka”, hata pengine “na kwa hakika utakuwa baraka”. Katika matukio yote, amri hii inaweka alama muhimu wa wazo la utafsiri. Inaondoa umakini kutoka kwa Abrahamu kupokea baraka (kama tulivyoona katika nusu ya sehemu ya kifungu cha 2) Kwa Abrahamu kuwa mfereji wa baraka kwa wengine.

Sehemu hii ya pili ya umbo la amri inafuatiwa pia na maelezo ya vitenzi vitatu huru. Vitenzi hivi vitatu vinaonesha maendeleo ambayo Abrahamu angekuwa baraka kwa wengine. Kwanza, Mungu alisema, “Nitawabariki wakubarikio …” Maana yake, Mungu angelitoa mambo mazuri kwa wale waliofanya vizuri kwa Abrahamu. Wakati watu wakimfanyia Abrahamu mambo mazuri, Mungu atawafanyia mambo mazuri. Pili, Mungu aliahidi, “atakaye kulaani, nitamlaani, …” Maana yake, Mungu angewalaani wale ambao watakaomfanyia Abrahamu jeuri. Mungu aliahidi kumlinda Abrahamu kutokana na madhara kwa mwitikio wa ukali kwa wale ambao walijifanya kuwa maadui wa Abrahamu. Lakini katika nafasi ya tatu, Mungu alisema, “watu wote … watabarikiwa kupitia wewe”. Katika mtazamo wa kwanza, huu mlengo wa tatu unaelekea kupinga usemi wa kulaani kwa maadui wa Abrahamu, lakini Mungu alimwahidi Abrahamu kuwa kwa maana ya mchakato wa kuwabariki marafiki wa Abrahamu na kuwalaani maadui zake, Mungu angelipanua baraka zake zaidi kwa familia zote za ulimwengu. Kwa hiyo, tunaona kuwa sarufi ya kufungua Mwanzo sura 12 inagawanyika katika sehemu tatu kuu: utangulizi, unaolenga baraka za Mungu kuufikia ulimwengu wote kupitia Abrahamu.

Kuelewa muundo wa vifungu hivi katika Mwanzo sura 12 ni muhimu kwa sababu katika mambo mengi, habari za Abrahamu katika Mwanzo zinaonesha jinsi gani ahadi hizi Mungu alizozifanya kwa Abrahamu zilitimizwa katika maisha yake. Kama Musa alivyoandika juu ya mababu au wazee, imeweka umbo katika habari zake katika njia ambazo zilileta uangalifu kwa maneno ambayo Mungu alisema kwa Abrahamu alivyomwita kwenye Nchi ya Ahadi.

Pamoja na muundo wa sarufi hizi katika mawazo, tuko tayari kuona jinsi mada kuu ya maisha ya Abrahamu yanavyofunguka kutoka Mwanzo sura ya 12:1-3.

Yanayofunuliwa

Tutakumbuka kwamba, kuna mada kuu nne ambazo zinaonekana katika vifungu hivi. Tutaanza na baraka ya Mungu kwa Abrahamu. Baadae tutaendelea na mahitaji ya uaminifu wa Abrahamu kwa Mungu, halafu baraka za Mungu kwa Abrahamu, na mwisho baraka za Mungu kupitia Abrahamu.

Neema ya Kiungu

Wazo la kwanza, linalotokea mara nyingi katika maisha ya Abrahamu ni kwamba, uhusiano wa Mungu na Abrahamu ulikuwa katika msingi wa neema yake. Neema ya Mungu inaonekana katika maneno ya utangulizi wa sura ya 12:1. Kama tulivyoona, hapo tunasoma maneno haya:

Bwana akamwambia Abram (Mwanzo 12:1).

Maneno haya rahisi yalimkumbusha Musa asili ya wahusika wake kuwa, uhusiano wa Abrahamu na Mungu ulikuja kwasababu Mungu alikuwa ameingia katika maisha ya Abrahamu siku nyingi kabla ya Abrahamu kufanya kitu chochote katika huduma kwa Mungu. Wito wa Abrahamu ulikuja mapema sana katika maisha yake ya utu uzima. Alikuwa hajaondoka kwenda Kanani; alikuwa bado hajawashinda maadui; alikuwa bado hajajitoa kwenye ahadi kwa uaminifu; alikuwa hajawaombea uaminifu, alikuwa hajawaombea wale waaminifu kule Sodoma na Gomora; alikuwa hajashinda mtihani wowote wa imani. Kinyume chake, Mungu alimwita Abrahamu kama mtumishi wake maalumu kwasababu ilimpendeza Mungu kuwa na neema kwa Abrahamu.

Bila shaka, Neema ya Mungu haikuoneshwa tu katika hatua ya kwanza ya matembezi na Mungu. Neema ya Mungu ni mada ya Mungu ambayo inaonekana wakati wote wa habari ya matembezi ya Abrahamu, kwasababu Mungu alionesha huruma kwa wazee wakati wote katika maisha yake. Kwasababu Abrahamu alikuwa mwenye dhambi, Abrahamu alikuwa ni muhitaji wa huruma ya Mungu wakati wote. Kwa mfano, katika mstari unaojulikana sana katika Mwanzo 15:6 tunajifunza kuwa hata ukombozi wa haki wa Abrahamu ilikuwa zawadi ya huruma. Hapo tunasoma maneno haya:

Akamwambia Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki (Mwanzo 15:6).

Kama mtume Paulo alivyoonesha katika Warumi 4:3 na Wagalatia 3:6 ukweli ni kwamba, Mungu alimpa sifa pamoja na haki na hiyo ilionesha kwamba ni kitendo cha huruma, siyo zawadi ya matendo mema. Na ilikuwa kupitia neema ya Mungu na huruma ambayo Abrahamu alipokea na baraka zingine nyingi kutoka kwa Mungu.

Kama Wakristo, sote tunavyojua umuhimu wa neema ya Mungu katika maisha yetu. Tunajua kwamba Mungu huanzisha uhusiano wetu naye kwa neema na tunajua kuwa hutulinda sisi katika uhusiano wetu pamoja naye kwa neema yake. Tungekuwa wapi bila ya huruma ya Mungu? Ni vizuri, ni kitu kile kile kilichokuwa kweli kwa Abrahamu. Na zaidi ya hayo, neema ya Mungu ilikuwa pia muhimu kwa maisha ya Waisraeli kama Musa alivyoandika kuhusu Abrahamu. Nao pia walihitaji neema ya Mungu siku hadi siku katika maisha yao na kwa sababu hiyo, kama Musa alivyoandika habari za maisha ya Abrahamu, aliweka uangalifu mara kwa mara juu ya neema ya Mungu.

Uaminifu wa Abrahamu

Kwa kuongezea katika mada ya neema ya Mungu, tunapaswa pia kukumbuka kuwa Mwanzo sura 12:1-3 inasisitiza uaminifu wa Abrahamu. Mungu hakumchagua tu Abrahamu ili apokee neema yake; alionesha huruma kwa wazee au mababu ili kwamba Abrahamu aweze kuitikia kwa utii wa uaminifu. Kama ambavyo tumekwisha kuona, amri ya kwanza ya Mwanzo 12:1 inasisitiza wajibu wa kuwa mwaminifu kwa Bwana katika njia fulani Mungu alivyomwamuru hapo:

Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha (Mwanzo 12:1).

Haichukui muda kufikiri na kuona kuwa wito huu wa Mungu ulihitaji uaminifu mkubwa kutoka kwa Abrahamu. Alitakiwa kuacha nchi yake na mali ya baba yake na kwenda sehemu ambayo bado hajaoneshwa. Ndiyo, Mungu alionesha rehema kwa Abrahamu, lakini Abrahamu alitegemewa pia kuonesha uaminifu uliokuwandani, uaminifu wa kumtumikia Mungu.

La kusikitisha, Wakristo wengi huwa wanafikiri Abrahamu ni mfano tu wa imani na kumtumaini Mungu. Hii ni mada muhimu katika maisha ya Abrahamu na inaoneshwa katika vifungu kadhaa vya Agano Jipya. Lakini tusiache kuangalia kwa makini ukweli kwamba Mungu alimwamuru Abrahamu kuwa mtiifu, kumpa yeye huduma ya uaminifu. Mungu alihitaji uaminifu kutoka kwa wazee mara nyingi. Alikuwa awe mwaminifu kwa Mungu katika hali zote. Pengine mfano wenye kishindo kikubwa ni wakati ule Abrahamu alihitaji kuonesha uaminifu kwa Mungu katika Mwanzo sura ya 22, wakati ambapo alimwamuru mzee huyo kumtoa sadaka mwanae Isaka ili kuhakikisha kama alimpenda Mungu kuliko alivyompenda mwanae. Itakuwa vigumu kufikiria hitaji la juu kutoka kwa Mungu.

Ingawa Abrahamu alihitajika kuonesha uaminifu katika hili na katika njia nyingine nyingi, Mwanzo 12:1 inaonyesha wazi moja wapo ya wajibu mkubwa Abrahamu aliokuwa nao. Hapo Mungu alisema:

Uende mpaka nchi nitakayokuonyesha (Mwanzo 12:1).

Kama kifungu hiki kinavyoonesha, Abrahamu alihitajika kwenda katika nchi ambayo Mungu angelimwonesha yeye. Abrahamu angeliishi katika nchi ya ahadi, na mada hii inaonekana mara nyingi ndani ya habari kuhusu wazee. Ilikuwa muhimu sana katika mpango mkubwa wa Mungu, wote kwa Abrahamu na kwa mababu zao waaminifu kwamba wazee wote kwenye Nchi ya Ahadi. Na tunapokumbuka kuwa Musa aliandika habari hizi kuhusu Abrahamu kwaajili ya Waisraeli ambao alikuwa akiwaongoza kuelekea kwenye Nchi ya Ahadi, siyo jambo la kushangaza hata kidogo kuona msisitizo huu.

Kama wafuasi wa Kristo, tunaelewa kuwa, ingawa wokovu ni kipawa cha bure kitokanacho na neema ya Mungu, Mungu anategemea sisi tuoneshe shukrani kwake kwa kufanya juhudi kuzitii amri zake. Musa aliilewa kanuni hii pia. Alijua kwamba neema ya Mungu kwa Abrahamu ilimwongoza Abrahamu kuwa mwaminifu kwa Mungu. Na kwa sababu hiyo, tunaenda kuona kuwa, hitaji la uaminifu linaonekana mara nyingi sana katika kujifunza juu ya maisha ya Abrahamu. Musa alijua kitu fulani juu ya asili ya wahusika wa Israeli. Walikuwa wakikabiliwa na kusahau umuhimu wa kuishi katika maisha ya uaminifu mbele za Mungu. Ingawaje Mungu alikuwa amewaonesha huruma nyingi alipowaokoa kutoka Misri na kuwalinda jangwani, wakayageuka maagizo ya Mungu. Na kwa sababu hiyo, moja wapo ya mada kuu katika habari za Abrahamu likuwa uaminifu wa Abrahamu kwa Mungu. Mada hii inaonekana mara nyingi kwa sababu ya wahusika wa asili wa Musa, pamoja na sisi pia, tunahitaji kuhamasishwa kumtumikia Mungu katika utii kwa uaminifu.

Baraka kwa Abrahamu

Kama ambavyo tumekwisha kuona mpaka sasa, Mungu alionesha neema nyingi kwa Abrahamu, na alihitaji uaminifu wa kujitoa kutoka kwake, Mada hii ya tatu tunapaswa kuangalia katika Mwanzo 2:1-3 ni baraka iliyotolewa kwa Abrahamu. Utakumbuka kwamba Mungu alisema hiki kwa Babu katika Mwanzo 12:2:

Nami nitakufanya wewe uwe taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako, nawe uwe baraka (Mwanzo 12:2).

Mungu alitoa baraka tatu kwa Babu huyu. Katika nafasi ya kwanza, Mungu alisema kuwa, Abrahamu angekuwa taifa kubwa. Kiazi chake kingekuwa zaidi katika idadi. Na uzao wake kweli wangekuwa himaya, yaani taifa kubwa. Wakati ule Abrahamu na wale aliokuwa nao walikuwa wachache katika idadi. Na Abrahamu hakuwa na watoto wa kwake. Lakini bado, Mungu alimwahidi kuwa idadi ya wajukuu wa Abrahamu wangekuwa siku moja kuwa zaidi ya nyota katika anga.

Katika sehemu ya pili, Mungu alimwambia Abrahamu kuwa angelimbariki. Katika uwezekano wote, maelezo haya yanamanisha kuwa, Abrahamu na uzao wake wangepokea baraka ya mafanikio makubwa. Abrahamu na uzao wake wangeliishi katika afya nzuri na mafanikio. Wasingekuwa watu wa kutangatanga hapa duniani, wala wasingekuwa walowezi. Kwakuwa Abrahamu na watoto wake aliaminika kuwa waaminifu, wangeliyafurahia mafanikio makubwa.

Katika sehemu ya tatu, Mungu anatoa baraka inayohusu kipawa cha jina kubwa kwa Abrahamu. Katika maneno mengine, kama Abrahamu angalienda katika Nchi ya Ahadi na kumtumikia Mungu kwa uaminifu, idadi kubwa na umaarufu wa kizazi chake, wangelimfanya yeye, na wao, waheshimiwe duniani kote. Utukufu mkuu ungekuja kwa mababu na kwa uzao wake ulio mwaminifu.

Kwa kweli, katika habari zote za Abrahamu, Musa alionesha mara nyingi kuwa aina ya baraka hizi zilimwagwa kwa Abrahamu. Abrahamu alikuwa na watoto; alipata utajiri alipoenda kutoka uzoefu mmoja hadi mwingine. Alikuwa mtu aliyejulikana katika sehemu hiyo. Kwa Waisraeli waliosikia habari hizi, baraka za Ibrahiku zilileta matumaini makubwa kwa muda ujao pia. Zawadi ya uzao wake, mafanikio na umarufu uliotolewa kwa mababu ulionesha zawadi kubwa Mungu angelimpa Abrahamu kwa ajili ya uaminifu kwa uzao wake.

Sisi Wakristo, tumekwisha kupokea baraka nyingi sana kutoka kwa Mungu ambazo ni vigumu kuzihesabu zote. Na bila shaka, Waisraeli waliomfuata Musa kuelekea Nchi ya Ahadi walipokea pia baraka zisizoweza kuhesabika kutoka kwa Mungu. Waliokolewa kutoka utumwani; waliongezeka katika idadi; walilindwa na kutunzwa wakati wote katika safari yao yote na walipokuwa katika njia ya kuelekea nchi ya ahadi, na kuwa Mungu amewafanyia na kile kilichokuwa katika hazina kwa ajili yao. Kwa hiyo Musa aliandika kuhusu baraka za Mungu kwa Abrahamu kuwakumbusha wahusika wa Waisraeli wake zile baraka ambazo Mungu aliwapa katika maisha yao ili mioyo yao ijazwe na shukrani.

Baraka kupitia Abrahamu

Kwa kuongezea katika huruma ya Mungu, uaminifu wa Abrahamu, na baraka za Mungu kwa Abrahamu, Mwanzo 12:1-3 pia zinatupa angalizo katika ukweli kuwa baraka zingekuja kupitia Abrahamu kwa watu wengine. Kumbuka Mungu alisema nini katika Mwanzo 12:2-3:

Nami nitakufanya kuwa taifa kubwa, na kukubariki, kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia zitabarikiwa (Mwanzo 12:2-3).

Maneno haya yalieleza kuwa Abrahamu asingepokea baraka tu, lakini watu wote duniani watabarikiwa kupitia yeye. Mungu hakumwita Abrahamu kwenda nchi ya ahadi siyo kumtajirisha yeye na maisha yake na vizazi vyake tu, bali alimwita kuwa mfereji wa baraka za Mungu kwa familia zote za ulimwengu. Sasa ni muhimu kukumbuka kuwa kifungu hiki kinafundisha kuwa baraka za Abrahamu kwa dunia yote zingekuja kwetu katika njia mbili. Katika Mwanzo 12:3 Mungu alisema:

Nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa (Mwanzo 12:3).

Kufuatana na kifungu hiki, Abrahamu angelitumika kama upanga ukatao kuwili kati ya wanadamu. Kwa sababu Abrahamu alipewa upendeleo na Mungu, wakati watu kutoka mataifa mengine walipombariki Abrahamu, maana yake ni kwamba, walipomheshimu na kwa hiyo walimheshimu Mungu aliyekuwa anamtumikia, badaye Mungu angeliwabariki. Lakini watu wa mataifa walipomlaani Abrahamu na kumtenda jeuri, Mungu wa Abrahamu aliwaadhibu. Hatima ya watu wengine ilitegemea na jinsi gani walimfanyia Abrahamu.

Katika maisha ya wakati wake, Abrahamu alikutana na watu wengi akiwasilisha mataifa mengine kama Wafilisti, Wakanani, Wamisiri, na binamu yake Lutu, aliyekuwa baba wa Wamoabi na Waamoni. Mwingiliano huu ulikuwa wa kweli, kwa sababu walionesha njia maalumu ambazo Mungu alitunza neno lake la kuwabariki na kuwalaani watu wengine kutegemea na jinsi walivyomfanyia Abrahamu. Walionesha pia kuwa, hata katika wakati wa maisha yake, Abrahamu alianza kuwa wa baraka katika ulimwengu.

Mara nyingi sana, ni rahisi kwa watu wa Mungu kusahau mafundisho haya muhimu. Waisraeli katika siku za Musa, walikuwa kama Wakristo wengi wanaoishi leo. Tunafurahia baraka za wokovu na maisha kutoka kwa Mungu, lakini tunasahau kwa nini baraka hizi zimetolewa kwa kila mmoja wetu. Kila baraka Mungu aliyowapa Israeli chini ya uongozi wa Musa na kila baraka alizolipa kanisa lake leo,zipo kuwaajili ya kusudi kubwa. Tumebarikiwa ili tuweze kuzieneza baraka za Mungu kote duniani. Mungu alimwita Abrahamu kwake, ili Abrahamu ayaongoze mataifa ya ulimwengu katika baraka za Mungu. Mungu alimwita Israeli kwake katika siku za Musa ili wayaongoze mataifa ya ulimwengu katika baraka za Mungu. Na Mungu ameliita kanisa kwake leo ili tuweze kuyaongoza mataifa ya ulimwengu katika baraka za Mungu. Mada hii ilikuwa ya muhimu sana kwa Waisraeli waliopokea kwanza habari za Abrahamu. Na ni muhimu kwetu sisi pia tunapomfuata Kristo katika siku zetu.

HITIMISHO

Katika somo hili tumejadili mtazamo wetu wa kwanza katika maelezo ya jumla ya maisha ya Abrahamu. Na tumejikita katika kujadili muundo, au ubunifu wetu wa sehemu hii ya Mwanzo. Na tumepima mada kuu, au yaliyomo ambayo Musa alieleza katika maisha ya Abrahamu, na katika mazingira ya muundo wa kifasihi.

Tunavyoendelea mbele katika masomo haya, tutarudi katika mada za masomo haya kwa wakati mwingine tena. Tumeona kuwa habari ya maisha ya Abrahamu yana hatua tano zenye ulinganifu. Na pia tumeona kuwa, kuna mada nne kuu katika maisha ya Abrahamu: Ukarimu wa Mungu kwa Abrahamu, uaminifu wa Abrahamu, baraka za Mungu kwa Abrahamu, na baraka za Mungu kupitia Abrahamu. Mada hizi hazitupatii tu ufahamu kuhusu maisha ya Abrahamu yalivyomaanisha wakati wa kwanza walipoandikiwa Waisraeli wa zama zile, lakini pia zinatupa uwezo wa kuhusisha sehemu hii ya Maandiko na maisha yetu ya sasa.

Dk. Richard L. Pratt, Jr. (Mwongozaji) ni Mwanzilishi na Raisi wa huduma za Third Millennium Ministries. Alitumika kama Professor wa Agano la Kale Reformed Theological Seminary kwa zaidi ya miaka 20, na alikuwa mwenyekiti wa idara ya Agano la Kale. Ni Mchungaji aliyewekewa mikono, Dk. Pratt anasafiri mara kwa mara kuinjilisha na kufundisha. Alisoma Westminster Theological Seminary, alipata shahada ya M.Div. kutoka Union Theological Seminary, na alipata shahada yake ya Th.D. katika mafunzo ya Agano la Kale kutoka Chuo kikuu cha Harvard University. Dk. Pratt ni mhariri wa Biblia ya NIV Spirit of the Reformation Study Bible na mtafsiri wa vitabu vya New Living Translation. Ameandika pia Makala na vitabu vingi, pamoja na Pray with Your Eyes Open, Every Thought Captive, Designed for Dignity, He Gave Us Stories, Commentary on 1 & 2 Chronicles and Commentary on 1 & 2 Corinthians.