<link rel="stylesheet" href="https://cdn.plyr.io/3.7.8/plyr.css" />
BETA You're previewing the new Nexus — a work in progress.
Toa
Back to CatalogPRHHistoria ya Awali
Historia ya Awali ·VideoTranslated from English

PRH-01 Dunia Nzuri

Read the full text

From the transcript

Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa naendesha gari nikafika mahali nikakuta gari moshi limeacha njia yake. Lilibaki mahali pale bila kwenda popote. Kama ujuavyo, gari moshi likiacha njia yake ambayo limetengenezewa ili lipite, huwa ni hatari na haliwezi kwenda popote lisipopita kwenye njia yake. Hali kadhalika, mwanzoni mwa nyakati, Mungu aliweka utaratibu, au njia ambayo uumbaji ulipaswa kuifuata, na njia hiyo ilielekeza kwenye hatima kuu ya utukufu kwa uumbaji wake. Lakini katika nyakati zote wanadamu wameshindwa kuifuata njia ambayo Mungu aliiweka kwaajili ya uumbaji wake. Tumeipotosha dunia na kuishia kwenye tatizo kubwa zaidi.

Katika mfululizo huu wa masomo, tutajifunza kuhusu njia ambayo Mungu aliiweka kwaajili ya uumbaji wake mwanzoni kabisa mwa historia ya ulimwengu. Kitu ambacho Wakristo huita “maagizo ya uumbaji.” Tutachunguza Mwanzo 1-11 ambayo hujulikana kama sehemu ya Historia ya Zama za Kale. Sura hizi za Biblia zitatusaidia kuona njia ya ajabu ambayo Mungu alitaka watu wa Israeli waifuate chini ya uongozi wa Musa. Pia zitatuonesha njia ambayo watu wake wanapaswa kuifuata hata leo.

Tumeliita somo letu la kwanza, “Ulimwengu Mkamilifu” kwasababu tutatilia mkazo Mwanzo 1:1-2:3, kifungu ambacho Musa anaeleza namna Mungu alivyoumba ulimwengu kwa mpangilio mkamilifu na ambao ulimfurahisha.

Kama tutakavyoona, ulimwengu huo ulitarajiwa au ulikuwa ni kivuli cha hatima ambayo Mungu aliwaandalia Israeli katika kipindi cha Musa. Hatima ambayo pia Mungu huwapitisha watu wake wote katika historia. Siyo tu kwamba inatuonesha namna mambo yalivyokuwa hapo mwanzo, bali pia namna maisha yanavyopaswa kuwa leo, na namna ulimwengu wetu utakavyokuwa mwishoni mwa kipindi tulichonacho.

Somo hili limegawanyika katika sehemu nne. Kwanza, tutawasilisha muhtasari wa historia ya zama za kale za Mwanzo 1-11. Pili, tutajikita zaidi katika Mwanzo 1:1-2:3, tukitazama muundo wake wa kiuandishi. Tatu, tutachunguza maana ya asili ya sehemu hii ya kitabu cha Mwanzo kwa dira ya muundo wake. Na nne, tutatafuta matumizi sahihi ya kifungu hiki kwa nyakati za sasa. Tuanze na muhtasari wa historia nzima ya zama za kale za kitabu cha Mwanzo 1-11.

Continue reading the full transcript