<link rel="stylesheet" href="https://cdn.plyr.io/3.7.8/plyr.css" />
BETA You're previewing the new Nexus — a work in progress.
Toa
Back to CatalogGOSMatendo ya Yesu
Matendo ya Yesu ·VideoTranslated from English

GOS-02 Habari Njema Kulingana na Mathayo

Read the full text

From the transcript

Mnamo mwaka 1919 Mfalme Albert wa Ubelgiji aliitembelea nchi ya Marekani kwa gari moshi. Alikuwa na ujuzi mwingi kuhusiana na vyombo vya moto, kwa hiyo kwa mwendo wa kilometa kama kumi na tano hivi alikuwa amevalia mavazi ya kihandisi na aliliendesha gari moshi hilo. Kwa kituo kilichofuata, makutano waliokuwa na furaha ya kumwona mfalme Albert, hawakufanikiwa kumwona, walitarajia kumwona akiwa amevalia mavazi ya aina fuiani, na kutenda kwa namna fulani. Hivyo hawakuweza kutambua kwamba yule mtu mrefu aliyekuwa amevalia sweta na kofia ndiye aliyekuwa mfalme wa Ubelgiji.

Kwa mtazamo unaofanana na mfano huo, Injili ya Mathayo inatueleza habari kama hiyo. Ni habari ya mfalme Yesu, mfalme wa Wayahudi. Lakini walio wengi kipindi kile hawakumtambua kwa sababu hakuonekana katika hali ambayo watu walivyoutarajia mwonekano wake kuwa, na hakutenda kama walivyotarajia atende. Alikuwa mfalme wa tofauti kabisa.

Hili ni somo la pili katika mfululizo wetu wa Vitabu vya Injili. Somo hili tumeliita “Injili kama Ilivyoandikwa na Mathayo,” maana tutajikita katika usikivu wetu kwenye injili ya kwanza, yaani kitabu cha Mathayo.

Kusoma kwetu kwa injili ya Mathayo kutakuwa katika sehemu kuu tatu. Katika sehemu ya kwanza, tutazingatia mazingira ya kitabu cha Mathayo. Sehemu ya pili, tutachunguza muundo na maudhui yake. Sehemu ya tatu na ya mwisho, tutayatazama mawazo makuu katika injili hii ya Mathayo. Hebu sasa tuanze na historia ya awali ya Injili hii kama ilivyoandikwa na Mathayo.

Watu wengi huniuliza, “Kwa nini ninahitaji kutoa maelezo haya ya kitamaduni kuhusu Biblia? Kwa nini nisisome tu Biblia katika tafsiri nzuri na kuona maana yake? Huwa ninapenda kusema kifungu bila muktadha wake ni kifungu kinachoweza kumaanisha cho chote. Tatizo ni kwamba vifungu vyote vya kale vimetolewa katika aina fuiani ya kihistoria, kiuandishi, kiuchimbuzi na utafiti wa kihistoria, muktadha wa kidini ambavyo vyote ni tofauti na vyetu tulivyo navyo sasa. Mtu mmoja aliwahi kusema, “Yaliyopita ni kama nchi ngeni, hufanya mambo tofauti huko.” Yaliyopita hutofautiana sana na yale yaliyopo sasa, kwa sababu ya mpaka mkubwa tulionao dhidi ya mabaki ya kihistoria, kusoma kwa kuona yaliyopita kwa kulinganisha na makisio yetu ya sasa, ni usomaji makini wa Kibiblia.

Continue reading the full transcript